text
stringlengths 3
16.2k
|
|---|
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti, baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
|
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA CHAMA cha Orange Democratic Movement (ODM) kimekana habari kuwa kimeanzisha mchakato wa kugura muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya, kikitaja taarifa hizo kama za uwongo. Kwenye taarifa kupitia akaunti yake ya mtandao wa X, chama hicho kinachoongozwa na Raila Odinga kimetaja barua inayodaiwa kwamba kiliandika kutangaza nia yake ya kuondoka muungano huo kama “feki”. ODM, kupitia taarifa hiyo iliyotiwa saini na Katibu Mkuu Edwin Sifuna, imeitaka umma na haswa wafuasi wao na wale wa Azimio , kupuuzilia mbali uvumi huo. “Ni bongo feki ambazo hutunga mambo feki,” chama hicho kikafafanua. Chama hicho kilitoa ufafanuzi huo baada ya barua hiyo kuzungushwa kwenye mitandao ya kijamii mnamo Alhamisi, Desemba 14, 2023 na kuzua gumzo kali miongoni mwa Wakenya. Kulingana na barua hiyo feki iliyoandikiwa Msajili wa Vyama vya Kisiasa Anne Nderitu, ODM ilitaja kutoaminiana miongoni mwa vyama tanzu kama sababu yake kuamua kuondoka Azimio. Barua hiyo ilichipuka baada ya kuibuka kwa tofauti kati ya wandani wa Bw Odinga na viongozi wa vyama tanzu katika muungano wa Azimio. Kwa mfano, aliyekuwa msemaji wa kikosi cha kampeni za urais za Bw Odinga Makau Mutua juzi aliwakaripia vikali Katibu Mkuu wa Jubilee Jeremiah Kioni na kiongozi wa Narc Kenya kwa kupinga ripoti ya Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (NADCO). Aliwataka kugura Azimio badala ya kuendelea kupinga ripoti hiyo ambayo sasa imewasilishwa rasmi katika Bunge la Kitaifa na Seneti. Bw Odinga na viongozi wa ODM wameonekana kuunga mkono mapendekezo ya ripoti hiyo ilhali Bi Karua, Bw Kioni na hata kiongozi wa DAP-Kenya, Eugene Wamalwa wameonekana kuipinga. Watatu hao wanasema hatua yao inatokana na hali kwamba mapendekezo kwenye ripoti hiyo yamefeli kutoa suluhu kwa changamoto ya kupanda kwa gharama ya maisha. “Nitachukulia maanani kauli yake ndugu yangu Kioni na wenzake katika vuguvugu la Kamwene endapo wataongoza maandamano katika eneo la Mlima Kenya. Kwa hivyo, wafyate au waondoke Azimio,” Profesa Mutua akisema kupitia mtandoa wa X, zamani, Twitter. Bw Kioni alikasirishwa na kauli hiyo na kumjibu Profesa Mutua na hivyo kuongeza joto katika muungano huo ambao umekabiliwa na changamoto kadhaa tangu Bw Odinga aliposhindwa na Rais William Ruto katika kinyang’anyiro cha urais 2022. “Inasikitisha kuwa malofa wengine wakiongozwa na Makau Mutua wameamua kutumia “maandamano” kama kigezo cha uaminifu kwa baadhi ya watu katika muungano wa Azimio,” Bw Kioni akasema akisisitiza kuwa Jubilee haitabanduka kutoka Azimio. Licha ya tofauti hizo, Bw Odinga na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta hawajashughulikia suala hilo. Bw Kenyatta ndiye kiongozi wa Baraza Kuu la muungano huo, ilhali Odinga ndiye kiongozi wake. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA JUMLA ya maafisa wa 37 wa usalama walikufa wakiwa kazini ndani ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita, kulingana na ripoti ya hivi punde kutoka kwa Wizara ya Usalama wa Ndani. Kulingana na ripoti hiyo iliyotolewa Alhamisi Desemba 14, 2023 maafisa hao wanaotoka vikosi vya polisi wa kawaida, polisi wa utawala (AP), idara ya magereza na Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) walikufa kati ya Novemba 22, 2022 na Novemba 23, 2023. Kati ya maafisa hao 37, 24 wanatoka Huduma ya Polisi Nchini (NPS), 10 wanatoka kitengo cha Huduma za Polisi wa Utawala, wawili wanatoka Huduma ya Magereza Nchini na mmoja anatoka idara ya DCI. Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki aliwaongoza maafisa kutoka vikosi hivyo katika Ibada ya Pamoja ya Ukumbusho wa maafisa hao waliopoteza maisha yao wakiwa kazini. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Polisi wa Utawala, Embakasi, Nairobi. Aidha, hafla hiyo pia ilihudhuriwa na familia za marehemu. Idadi kubwa ya maafisa wa polisi wameuawa au kujeruhiwa wakiwa katika harakati za kupambana na wahalifu. Maisha yao haswa yamo hatarini zaidi katika kaunti zilizoko Kaskazini Mashariki mwa Kenya kama vile Mandera, Wajir na Mandera zinazozongwa na mashambulio ya kila mara ya wanamgambo wa Al-Shabaab. Kumekuwa na visa vya maafisa wa usalama kuuawa baada ya magari yao kulipuliwa na vilipuzi vilivyotegwa ardhini (IED) katika kaunti hizo zinazokaribiana na mpaka wa Kenya na Somalia. Agosti 2023, Waziri Kindiki aliiambia Kamati ya Bunge kuhusu Usalama kwamba jumla ya maafisa 58 waliuawa na wahalifu wakiwa kazini tangu 2018. Mnamo Novemba 10, 2012 jumla ya maafisa 42 wa polisi waliuawa wakati mmoja walipokuwa wakiendesha operesheni ya kupambana na majangili katika bonde la Suguta lililoko eneo la Baragoi, Kaunti ya Samburu. Desemba, 2022 Waziri Kindiki alitangaza kuanzishwa kwa Hazina Maalum ya kusaidia familia za maafisa wa polisi na wale wa magereza waliokufa kazini. “Hazina hiyo inatarajiwa kukusanya pesa za kusaidia familia zilizofiwa kwa kulipia watoto wao karo, kugharamia huduma za afya miongoni mwa mahitaji mengine,” Profesa Kindiki akasema mnamo Desemba 15, 2022. Kimsingi, maafisa wa polisi huuawa na magaidi, majangili, wezi wa kimabavu, wenzao na hata raia. Hata hivyo, rekodi za polisi zinaonyesha kuwa idadi kubwa ya maafisa hao huuawa kwa kushambuliwa na majangili, haswa katika maeneo ya Kaskazini na Kaskazini Mashariki mwa Kenya. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA WANDERI KAMAU WAZIRI wa Uchukuzi, Bw Kipchumba Murkomen, sasa ameiondolea lawama Kampuni ya Kusambaza Nguvu za Umeme Nchini (KP), kutokana na mtindo wa umeme kupotea kila mara katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA), jijini Nairobi. Mnamo Alhamisi, Desemba 14, 2023 Bw Murkomen alitaja tatizo hilo kuchangiwa na miundomsingi duni ya kusambaza umeme katika uwanja huo. Waziri Murkomen pia alihusisha tatizo hilo na ukosefu wa motisha wa kutosha miongoni mwa wafanyakazi katika uwanja huo na Halmashauri ya Kusimamia Viwanja vya Ndege Kenya (KAA). “Matatizo ya umeme kupotea kila mara katika uwanja wa JKIA hayahusiani na utendakazi wa KP. Hili ni tatizo lililoanza zamani sana. Limekuwepo hata wakati wa serikali zilizopita,” akasema Bw Murkomen. Waziri huyo alisema kuwa tiba kuu kwa matatizo hayo ni utengenezaji na ulainishaji wa mitambo ya kusambaza umeme katika uwanja huo, wala si kuielekezea lawama KP kila wakati umeme unapopotea. “Ingawa kampuni ya Kenya Power ina changamoto zake, tatizo ambalo limekuwa likitokea katika JKIA linahusiana na usimamizi mbaya wa uwanja huo wenyewe wala si la taasisi ya nje,” akasema Bw Murkomen. Kwa muda mrefu, wasafiri ambao wamekuwa wakijipata gizani katika uwanja huo umeme unapopotea, wamekuwa wakiilaumu kampuni hiyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

Na CHARLES WASONGA WAKENYA wamepata afueni kidogo msimu huu wa sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya baada ya serikali kupunguza bei ya mafuta japo kwa kiwango kidogo. Mamlaka ya Kusimamia Sekta ya Kawi na Mafuta (EPRA) imepunguza bei ya petroli kwa Sh5 kwa lita huku ikishusha bei ya dizeli na mafuta taa kwa Sh2 na Sh4, mtawalia. Hii ina maana kuwa kuanzia Desemba 15 bei ya petroli itauzwa Sh212.36 kwa lita jijini Nairobi na viunga vyake kutoka bei ya sasa ya Sh217.36. Nayo dizeli itauzwa kuwa Sh201.47 na mafuta taa ikiuzwa kwa Sh199.05, kutoka bei ya Sh203.47 na Sh203.06, mtawalia. Bei hizo zitatumika kwa kipindi cha mwezi mmoja hadi Januari 14, usiku wa manane. Bei ya bidhaa hizi katika maeneo mengine nchini zitagemea umbali kutoka Mombasa ambako shehena za bidhaa hizo hushuka kutoka ng’ambo. “Bei hizo mpya zinajumuisha ushuri wa VAT wa kima cha asilimia 16 kulingana na Sheria ya Fedha na Sheria za Ushuru ya 2020. Aidha, zinajumuisha ushuru wa bidhaa uliyoanishwa na mfumko wa bei kulinga na hitaji la notisi ya kisheria nambari 194 ya 2020,” Epra ikasema Alhamisi jioni kwenye taarifa kwa vyombo vya habari. Mamlaka hiyo ilieleza kuwa punguzo hilo la bei ya mafuta linatokana na kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo katika masoko ya kimataifa. Kwa mfano, kulingana na Epra, bei ya petroli ilipungua kwa kima cha asilimia 16.11 kutoka dola 827.75 za Amerika (Sh125,818) kwa pipa mnamo Oktoba, 2023 hadi dola 694.44 (Sh105,554) mwezi wa Novemba 2023. Ni kutokana na kupungua huku kwa bei ya bidhaa hizi katika masoko ya kimataifa ambapo juzi kiongozi wa upinzani Raila Odinga aliishinikiza serikali kushusha bei kwa kiwango cha kati ya Sh48 hadi Sh50 kwa lita. “Tuko na habari kwamba bei ya mafuta kule nje imeshuka kwa kiwango kikubwa zaidi. Kwa hivyo, sisi kama Azimio hatutaki serikali kupunguza bei Sh5 bali tunataka ipunguze bei kwa hadi Sh50 kwa lita moja,” akasema akiwa kaunti ya Kajiado. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA TITUS OMINDE Naftali Kinuthia, 33, aliyepatikana na hatia ya kuua mpenzi wake baada ya kutoalikwa kwa sherehe ya siku ya kuzaliwa, Alhamisi Desemba 14, 2023 amefungwa jela miaka 40 kwa kosa hilo. Jaji Stephen Githinji alisema kwenye uamuzi wake kwamba, kutoalikwa kwenye sherehe kama hiyo haikuwa sababu tosha ya kumuua mpenzi. Kwenye tukio hilo mwaka 2019, Kinuthia alifika nje ya kitivo cha utabibu cha chuo kikuu cha Moi mjini Eldoret akiwa na shoka. Wakati wa kujitetea kortini, Kinuthia alisema wakati mmoja alitumia zaidi ya Sh200,000 kwa Ivy Wangeci, ambaye walikuwa marafiki tangu utotoni walipokuwa shule ya msingi moja mjini Thika. Aliendelea kumfadhili Wangeci hata baada ya kuwa mbali naye. Aliambia mahakama kuwa, alipatwa na hasira alipoona mpenzi wake akikumbatia mwanaume mwingine. Alikasirika kuwa Bi Wangeci aliendelea kukusanya pesa kutoka kwake, ilhali hakuwa na nia ya kuendelea na uhusiano wa kimapenzi na yeye. Alimwambia Jaji Githinji kwamba, kabla ya kuchukua uamuzi wa kumuua, alikuwa amemtumia Sh7,000 kwa siku yake ya kuzaliwa, lakini hakuwa amemwalika kwenye sherehe. Hakukasirika, alisema, kwa sababu amekuwa akimfadhili kwa miaka mingi ili kulinda uhusiano. Kilichomuudhi ni Ivy kumkumbatia mwanaume mwingine mbele yake. Kupitia kwa wakili wake, Wokabi Mathenge, mwanaume huyo alielezea kujutia kosa alilotenda, na kuiambia mahakama kuwa amebadilika kwa muda wa miaka minne aliyokuwa rumande. Mwanume huyo, 33, alikamatwa baada ya kumshambulia kwa shoka mpenzi wake ambaye wakati huo walikuwa wameachana. Kupitia kwa wakili wa familia Kiroko Ndegwa, familia ya marehemu ilikuwa imeomba mahakama kumwadhibu Bw Kinuthia kwa kifungo cha kunyongwa. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

Na RICHARD MUNGUTI ILIKUWA furaha na kilio katika mahakama ya Milimani pale aliyekuwa waziri wa fedha Henry Rotich na watu wengine nane walipoponyoka vifungo vya miaka na mikaka katika kashfa ya ujenzi wa mabwawa ya Arror na Kimwarer kwa gharama ya Sh63 bilioni. Bw Rotich alidondokwa na machozi sawia na washtakiwa wenzake hakimu mkuu Eunice Nyuttu aliposema “Hakuna ushahidi uliowasilishwa kuwezesha mahakama kuwasukuma kizimbani kujitetea.” Bi Nyuttu alikashifu afisi ya kiongozi wa mashtaka ya umma DPP kukwepa majukumu yake na kutowasilisha ushahidi kutoka kwa mashahidi 41 akiwamo waziri wa zamani wa kilimo Peter Munya. “Viongozi wa mashtaka waliambia hii mahakama-hatuna maswali kwa mashahidi hawa 41 kati ya mashahidi 49,” alisema Bi Nyuttu. Hakimu alisema DPP alikosa kutumia ipasavyo mamlaka aliyopewa katika kifungu 157 cha katiba na kuletea mahakama na umma wa Kenya fedheha. Akiwaachilia Bw Rotich huru, hakimu mkuu wa mahakama ya kuamua kei za ufisadi Bi Eunice Nyuttu alisema “upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha mashtaka 19 dhidi ya washtakiwa.” “Hakuna ushahidi uliowasilishwa katika kesi hii kuthibitisha upunjaji wa zaidi ya Sh63 bilioni dhidi ya washtakiwa wote,” alisema Bi Nyuttu. Hakimu huyo aliwakashfu viongozi wa mashtaka aliosema “walihepa kesi hiyo na kukataa kuwasilisha ushahidi wa mashahidi 41.” Akasema Bi Nyuttu:“Wakati kiongozi wa mashtaka Taib Ali Taib alipotoa taarifa yake ya kwanza alisema ushahidi utawasilishwa kuthibitisha jinsi washtakiwa walikula njama za kuipunja serikali Sh80 bilioni katika kashfa hiyo ya ujenzi wa mabwawa ya Arror na Kimwarer.” Akimnukuu Bw Taib, Bi Nyuttu alisema kiongozi huyo wa mashtaka alisema “upande wa mashtaka utathibitisha jinsi kampuni ambayo haikuwa imesajiliwa ilishinda tenda ya ujenzi wa mabwawa hayo mawili ya Arror na Kimwarer.” Hakimu alieleza kiongozi huyo wa mashtaka alisema ushahidi wa kushtua utawasilishwa jinsi pesa za umma zilianza kulipwa hata kabla ya ujenzi wa mabwawa hayo kuanza. Bi Nyuttu alisema baada ya mashahidi wanane kutoa ushahidi viongozi wa mashtaka walianza kukwepa kuwasilisha ushahidi kwa lengo la “kutafuta jinsi washtakiwa wataachiliwa huru na mahakama.” Hakimu alisema tabia hii ya viongozi wa mashtakiwa ilifedhehesha mahakama na washtakiwa aliosema wamekuwa kortini kwa muda mrefu wakisubiri kupata haki. Lakini hakimu alisema washtakiwa waliowakilishwa na mawakili Kioko Kilukumi, Katwa Kigen na Philip Nyachoti “hawakutendewa haki kamwe ila viongozi wa mashtaka walianza mchezo wa paka na panya kwa kuleta mashahidi na kutowauliza maswali.” Katika kesi hiyo, Bw Rotich alishtakiwa pamoja na Nyakundi Nyachiro, Jackson Njau Kinyanjui, David Kipchumba Kimosop, William Kipkemboi Maina, Paul Kipkoech Serem, Francis Chepkonga Kipkech, Titus Muriithi na Geoffrey Mwangi Wahungu. Walikabiliwa na mashtaka ya kutumia mamlaka ya afisi zao vibaya katika ujenzi wa Arror na Kimwarer. Washtakiwa hao tisa walikana shtaka la pamoja la kula njama za kuilaghai Serikali ya Kenya Dola za Marekani ($) 501,829,769 kwa kuidhinisha ujenzi wa mabwawa haya ya Kimwarer na Arror kabla ya kujadiliwa na kupitisha na asasi husika za serikali. Walishtakiwa kuzipa kampuni za Italia ujenzi wa miradi hiyo kinyume cha sheria. Hakimu alisema kampuni hizo Cooperativa Muratori & Cementisti (CMC di Ravenna) na Itinera S.p.A zilipewa kandarasi hiyo. Mahakama ilisema hoja kuhusu kandarasi hiyo ziliibuka na zabuni hiyo ikapigwa kalamu ndipo serikali ikashtakiwa katika jopo la kimataifa na kampuni hizo. Kampuni hizo ziliomba zilipwe kitita cha Sh80 bilioni. Mahakama ilisema mamlaka ya KVDA ilitoa idhini ya ujenzi huo iliyosema haukuwa umesukwa kwa mujibu wa sheria. Hata hivyo mahakama ilisema afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma haikuwasilisha ushahidi kuthibitisha mashtaka 19 dhidi ya washtakiwa iliowaachilia huru. Bi Nyuttu aliamuru washtakiwa warudishiwe dhamana zao. Pia aliamuru uamuzi wake upelekewe asasi husika za serikali zikajadili njia za kuwaadhibu viongozi wa mashtaka waliokwepa kesi hiyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

WASHINGTON, MAREKANI NA MASHIRIKA RAIS wa Marekani Joe Biden alisema siku ya Jumanne kwamba Israel inapoteza uungwaji mkono na mataifa mengi duniani kutokana na mashambulizi yake ya “kiholela” dhidi ya Gaza. Wakati huo, jeshi la Israel lilisema wanajeshi wake 10 waliuawa ukanda wa Gaza. Biden alisema Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu anapaswa kubadilika, na kufichua mpasuko mpya katika uhusiano na waziri mkuu wa Israel. Matamshi ya Biden, aliyoyatoa kwa wafadhili katika kampeni yake ya kuchaguliwa tena kwa mwaka wa 2024, yalikuwa muhimu zaidi kwake hadi leo ya jinsi Netanyahu alivyoshughulikia vita vya Israeli Gaza. Ni tofauti kabisa na kumbatio lake halisi na la kisiasa kwa kiongozi wa Israel siku chache baada ya mashambulizi ya wanamgambo wa Hamas lililofanyika Oktoba 7 kusini mwa Israel. “Usalama wa Israel unaweza kukaa Marekani, lakini sasa hivi ina zaidi ya Marekani. Ina Umoja wa Ulaya, ina Ulaya, ina sehemu kubwa ya dunia … Lakini wanaanza kupoteza uungwaji mkono huo kwa sababu ya kupiga mabomu ya kiholela ambayo hufanyika Hamas,” Biden alisema. Kulipiza kisasi kwa Israel dhidi ya mashambulizi ya Hamas kumesababisha vifo vya watu 18,000, maafisa wa Gaza wanasema, na kujeruhi 50,000, na kusababisha mahangaiko ya kibinadamu. Matamshi ya Biden yalifungua dirisha jipya katika mazungumzo yake ya faragha na Netanyahu, ambaye wamekuwa na kutoelewana kwa kina kwa miongo kadhaa. Biden aligusia mazungumzo ya faragha ambapo kiongozi huyo wa Israel alisema: “‘Wewe uliyepiga kwa zulia Ujerumani, ulirusha bomu la atomi, raia wengi walikufa.” Biden alijibu: “Ndio, ndio maana taasisi hizi zote zilianzishwa baada ya Vita vya Pili vya Dunia ili kuhakikisha kwamba haikutokea tena … usifanye makosa kama tuliyofanya mnamo 9/11. Hakuna sababu tulivyolazimika kuwa katika vita nchini Afghanistan.” Biden, ambaye mara nyingi huzungumza kwa hasira kwenye hafla zake za kuchangisha pesa, alionekana katika hoteli ya Washington na takriban watu mia moja, pamoja na idadi ya Wayahudi waliohudhuria. Alitambulishwa na kiongozi wa muda mrefu ndani ya Kamati ya Masuala ya Umma ya Israel ya Marekani, inayoiunga mkono Israel. Maoni makali ya Biden yalienda sambamba na mshauri wa usalama wa taifa wa White House, Jake Sullivan akijiandaa kwenda Israel kwa mazungumzo na baraza la mawaziri la vita la Israel. Netanyahu alisema katika taarifa yake Jumanne kwamba Israel imepokea “uungwaji mkono kamili” kutoka kwa Marekani kwa uvamizi wake wa ardhini Gaza na kwamba Washington imezuia “shinikizo la kimataifa la kusitisha vita.”
|
Tags
|
You can share this post!
|
Previous article
|
Mcheshi anayewapa tumbojoto wanasiasa Mlima Kenya kwa...
|
Next article
|
Hakimu aeleza kusikitishwa kwake huku akiachilia Rotich na...
|
T L
|
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA WAZIRI wa Kawi Davis Chirchir ameorodheshwa kama waziri mwenye utendakazi duni zaidi miongoni mwa Mawaziri wote 22 katika serikali ya Rais William Ruto. Hii ni kulingana na matokeo ya utafiti ulioendeshwa na kampuni ya Trends and Insights for Africa (TIFA) yaliyotolewa rasmi Jumatano, Desemba 13, 2024. Bw Chirchir ambaye amekuwa akielekezewa lawama na umma kutokana na kupandishwa kwa bei ya mafuta na visa vya kupotea ghafla kwa stima, aliandikisha utendakazi wa asimilia 19. Katika safu hiyo ya chini kiutendakazi, pia waliorodheshwa Waziri wa Jinsia Aisha Jumwa (aliyewakilisha kiwango cha utendakazi cha asilimia 23) na Waziri wa Fedha Profesa Njoroge Ndung’u akiwa wa tatu kwa utendakaz wa chini kwa kupata asilimia 24. Waziri wa Maji, Zacharia Njeru na mwenzake wa Ardhi Alice Wahome pia waliandikisha kiwango sawa cha asilimia 24. Waziri wengine walioko kwenye orodha ya mawaziri 10 wenye utendakazi duni ni pamoja na; Florence Bore wa Leba (asilimia 25 ), Rebecca Miano wa Biashara (asimilia 27), Moses Kuria wa Utumishi wa Umma (asilimia 27), Peninah Malonza wa Jumuiya ya Afrika Mashariki- EAC (asilimia 27), na Simon Chelugui wa Ustawi wa Vyama vya Ushirika (asimilia 31). Jumatatu, Desemba 11, Bw Chirchir alikabiliwa na wakati mgumu alipotakiwa kuelezea sababu ya kutokea kwa kisa cha tatu cha kupotea kwa kawi kote nchini siku iliyotangulia (Jumapili) mwendo wa saa mbili za usiku. Tatizo hilo lililodumu kwa zaidi ya saa sita, piailiathiri Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA). Hii ni baada ya jenereta ya kuzalisha kawi ya stima ya ziada nyakati za dharura kufeli kufanyakazi. Hicho kilikuwa ni kisa cha pili cha kupotea kwa stima kote nchini tangu Rais William Ruto alipoingia mamlakani Septemba 13, 2022. Kando nayo, Wakenya wamekuwa wakilalamikia kupanda kwa bei ya mafuta ambayo sasa inauzwa Sh217.36 (petroli), Sh203.47 (dizeli) na Sh203.06 (mafuta taa). Aidha, Waziri Chirchir amelaumiwa kuhusiana na mvutano kuhusu umiliki wa shehena ya dizeli ya thamani ya Sh17 bilioni iliyonaswa katika Bahari Hindi ikiletwa nchini. Mfanyabiashara kwa jina Anne Njeri Njoroge alidai kuwa shehena hiyo ilikuwa mali yake. Mvutano huo bado unachunguzwa na asasi husika za serikali pamoja na Kamati ya Bunge la Kitaifa kuhusu Kawi inayoongozwa na Mbunge wa Mwala, Vincent Musyoka, maarufu kama Kawaya. Wakati huo huo, Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki bado amesalia kidedea kama Waziri mchapakazi zaidi katika serikali ya Rais Ruto. Alisifiwa na asilimia 65 ya jumla ya watu 3,009 waliohojiwa katika utafiti huo uliofanywa kati ya Novemba 25, 2023 na Desemba 7, 2023. Mahojiano yalifanywa kwa njia ya simu na kwa kutumia lugha za Kiswahili na Kiingereza. Profesa Kindiki anafuatwa na Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi (asilimia 62), Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu (asilimia 58), Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen na mwenzake wa Afya Susan Nakhumicha wamepata asilimia 57. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA BENSON MATHEKA HATUA ya viongozi wa mataifa jirani na ya kigeni kukosa kuhudhuria sherehe za Jamhuri Dei jijini Nairobi imeibua maswali kuhusu mtizamo wao kuhusu sera za serikali ya Kenya Kwanza. Hali hii ni tofauti na Rais William Ruto ambaye amekuwa akitumia mialiko anayopata kuzuru mataifa mbali mbali jirani, Afrika na ng’ambo.
|
Mnamo Jumapili, serikali kupitia Katibu wa Masuala ya Ndani Dkt Raymond Omollo ilitangaza kuwa viongozi watatu wa nchi za kigeni wangehudhuria maadhimisho ya 60 ya Jamhuri Dei katika bustani ya Uhuru Gardens, Nairobi.
|
Japo hakutaja viongozi hao na nchi zao, ilitarajiwa kuwa angalau wangetoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambayo mbali na kuwa jirani, nchi hizo zimeunganika na Kenya kiuchumi na kijamii.
|
Hata hivyo, hakuna hata kiongozi mmoja wa nchi hizo aliyehudhuria sherehe hizo akiwemo mwenyekiti wa EAC,l Rais Salvar Kiir wa Sudan Kusini.
|
Rais wa Belarus Aleksandr Lukashenko aliyezuru nchini Jumatatu jioni pia hakuhudhuria sherehe hizo.
|
Kulingana na Shirika la Utangazaji la Kenya (KBC), Rais Lukashenko alikutana na Rais Ruto katika ikulu ya Nairobi na alitarajiwa kuhudhuria sherehe za Jamhuri jana.
|
“Rais wa Belarus Aleksandr Lukashenko na mwenzake wa Ethiopia Sahle Work Zewde tayari wamewasili nchini kama wageni wa Rais William Ruto katika sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya uhuru,” KBC ilisema katika taarifa mtandaoni Hata hivyo, Ikulu haikuthibitisha iwapo alikuwa amealikwa kwa sherehe hizo na
|
hakufika katika bustani ya Uhuru Gardens ambapo ziliandaliwa.
|
Baadhi ya viongozi wa mataifa jirani waliwatuma maafisa wa ngazi za chini kuwawakilisha tofauti na Rais Ruto anayependa kuhudhuria binafsi mialiko katika nchi za kigeni.
|
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu alimtuma rais wa Zanzibar Ali Mwinyi ambaye alisema kiongozi huyo jirani wa Kenya upande wa kusini “ hakuweza kufika kwa kuwa nchi imegubikwa na mafuriko yanayosababishwa na mvua ya El Nino kaskazini mwa nchi yetu”.
|
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ambaye alialikwa kuhudhuria sherehe za jana alimtuma naibu waziri mkuu wa nchi hiyo Rebecca Kadaga huku Rais wa Burundi Jenerali Évariste Ndayishimiye akiwakilishwa na makamu wake Prosper Bazombanza.
|
Rais Museveni jana alikuwa akizindua sensa ya sita katika nchi yake. Marais wa nchi zingine za EAC Paul Kagame( Rwanda), Salvar Kiir( Sudan Kusini), Félix Antoine Tshisekedi (DRC) na Somalia Hassan Sheikh Mohamud hawakuhudhuria huku Ethiopia ikidumisha utamaduni wake wa kumtuma rais wake Sahle-Work Zewde kumwakilisha Waziri Mkuu Abiy Ahmed. Rais Zewde alisema amekuwa akihudhuria sherehe za Jamhuri jijini Nairobi kwa miaka minane.
|
Mtaalamu wa masuala ya kidiplomasia James Waki anasema si lazima viongozi wa nchi za kigeni wafike binafsi wanapoalikwa na mataifa mengine japo kufika kwao huwa kunasawiriwa kama ishara ya nia na heri njema.
|
“Mialiko hutumwa lakini uamuzi ni wa viongozi wanaoalikwa. Wanaweza kufika binafsi au kutuma ujumbe unaoongozwa na afisa wanayechagua. Hata hivyo kufika kwao binafsi huwa na uzito kwa kusawiri uhusiano wao na nchi inayowaalika una nguvu,” alisema.
|
Jana, Rais Ruto kwa mara nyingine alisisitiza kwamba, kuanzia Januari, Kenya itafungua milango yake kwa raia wa nchi za Afrika na hawatahitajika kuwa na viza kuingia nchini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA RAIS William Ruto ametangaza kuwa wakongwe, mayatima na walemavu wataanza kupokea malipo yao ya Sh2, 000 kila mwezi kutoka kwa serikali kupitia maduka ya M-Pesa kule vijijini. Mpango huo unaojulikana kama Inua Jamii ulianzishwa na utawala uliopita wa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta na unafaidi jumla ya watu milioni 1.2 waliosajiliwa rasmi. Kiongozi wa nchi alisema hayo Jumanne, Desemba 12, 2023 alipoongoza sherehe za 60 za Jamhuri Dei Uhuru Gardens, Nairobi “Sasa serikali imeamua kwamba wazee, mayatima na watu wanaoishi na ulemavu ambao hupokea pesa za mahitaji yao ya kimsingi kila mwezi chini ya mpango wa Inua Jamii, hawatatembea kwa mwendo mrefu. Wataweza kupata pesa hizo vijijini mwao kupitia maduka ya M-Pesa,” Rais Ruto akaeleza. Alisema mpango huo umewezeshwa kutokana na mkataba uliotiwa saini kati ya serikali na kampuni ya mawasiliano ya Safaricom. “Safaricom itatoa huduma hii bila malipo,” Rais Ruto akaeleza alipowahutubia Wakenya wakati wa maadhimisho ya Jamhuri Dei 2023. Dkt Ruto alisema mayatima ndio kundi la kwanza litakaloanza kufaidi kwa mpango huo mwishoni mwa mwezi huu wa Desemba. “Wakongwe na wale wengine wataanza kupokea pesa zao kupitia M-Pesa kuanzia mwishoni mwa Januari mwaka ujao, 2024, kwa sababu tunahitaji kufanya mambo fulani kwanza,” akaeleza. Dkt Ruto alikariri kwamba serikali yake inaendelea kutekeleza sera ambapo makundi hayo ya watu wenye mahitaji maalum hupokea malipo yao kabla ya watumishi wengine wa serikali kulipwa mishahara yao. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MHARIRI
|
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI
|
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI
|
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI
|
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI
|
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI
|
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI
|
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI
|
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI
|
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI
|
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini.
|
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI
|
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI
|
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
|
Na BENSON MATHEKA
|
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU
|
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA
|
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA
|
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA
|
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU
|
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA
|
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO
|
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI
|
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA
|
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON
|
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA
|
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
|
Na MASHIRIKA
|
LONDON, Uingereza
|
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB
|
WANASAYANSI wanachunguza kuhusu mchipuko wa virusi vipya vya corona aina ya Delta, katika nchi za Amerika, Uingereza,... Na MAUREEN ONGALA
|
MASAIBU ambayo wagonjwa wa Covid-19 hupitia katika kaunti za Pwani, yameanikwa wazi baada ya kifo cha afisa mkuu wa... SIAGO CECE na ANTHONY KITIMO
|
UFISADI miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali katika mpaka wa Kenya na Tanzania, umezidi kuwaweka... Na WAANDISHI WETU
|
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.